Soundcloud

Serena Williams na Andy Murray wazidi Kuwagalagaza wapinzani wao kwenye mashindano ya Wimbledon.


Wakati mnyukano ukiendelea kwenye mashindano ya tenisi ya ‘Wimbledon’ yanayofanyika jijini London nchini Uingereza,wakongwe Serena Williams na Andy Murray wamefanikiwa kutinga katika mzunguko wa pili wa mshindano hayo ambapo kwa upande wa Serena yeye amemchakaza Amra Sadikovic kwa seti 6-2,6-4 huku Murray akimchapa Liam Broady kwa seti 6-2 6-3 6-4 katika mchezo uliokuwa wa kukata na shoka.
serena wembledon 008Katika mzunguko wa pili Serena Williams atacheza dhidi ya Christina McHale huku Andy Murray mwenye miaka 29 akikipiga na Yen-Hsun Lu kutoka china.
Tennis - Aegon Championships - Queens Club, London - 20/6/15  Great Britain's Andy Murray in action during his semi final match  Action Images via Reuters / Paul Childs  Livepic


Post a Comment