Soundcloud

VIDEO:Common aachia video ya wimbo wa kupinga mauaji ya watu weusi Marekani

Rapper kutoka mji wa Chicago nchini Marekani, Common ameachia video
ya wimbo wake wa ‘Black America Again’ aliomshirikisha Stevie Wonder
ambao unaopinga mauaji ya watu weusi yanayoendelea nchini humo.common-epix


“Here we go again,” amerap Common kwenye wimbo huo. “Trayvon will
never grow to be an older man / Black children, they childhood stole
from them / Robbed of our names and our language, stole again.”
Wimbo huo utapatikana kwenye albamu ya 11 ya msanii huyo anayotarajia kuiachia hivi karibuni.


Mpaka sasa ni zaidi ya watu watano weusi wameuawa na polisi wa
kizungu nchini humo kuanzia mwezi Julai, mwaka huu akiwemo Philando
Castile, Alton Sterling na tukio jingine lililotokea siku chache
zilizopita kwenye mji wa Charlotte kwa Keith Lamont Scott kupigwa na
risasi