Soundcloud

Diamond Platnumz: Saida Karoli ana asilimia zake kwenye kila pesa ambayo ‘Salome’ itaingiza

Saida Karoli atanufaika na ‘Salome’ wimbo mpya wa Diamond ambao una vionjo kutoka kwenye wimbo wake wa ‘Chambua kama karanga’


Diamond amesema kuwa mwanamuziki huyo mwongwe wa nyimbo za asili ana asilimia 25 kwenye pesa ambazo wimbo huo utakuwa unaingiza,


“Kitu tulichokifanya kabla ya kurealise wimbo, tulizungumza na
uwongozi wake tukawaambia tunafanya ichi,ichi na ichi, kuna kiasi pia
tukakitoaili kiende kwake afu tukampa  25 percent ya publishing kila
income ya publishing ikiwa inaingia katika huu wimbo, mama atakuwa
anapata percent”
Diamond ameiambia Perfect 255.Saida Karoli alipata mafanikio makubwa kupitia wimbo huo ikiwa ni
pamoja na kutumika kwenye filamu ya muandaji maarufu wa Hollywood, Tyler
Perry.