Soundcloud

Kikwete ahutubia maelfu kwenye tamasha la Global Citizen fest ambalo pia Rihanna, Kendrick Lamar na Usher walitumbuiza

Rais mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete aliungana na maelfu ya
kuhudhulia tamasha la Global Citizen fest. lililofanyika New York,
Marekani.IMG_9834


Rais Mstafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Kamishna wa
Kamisheni ya Kimataifa kuhusu elimu akizungumza mbele ya umati wa wakazi
wa jiji la New York katika tamasha la Global Citizen Festival
lililofanyika Central Park. Kupitia tamasha hilo, Mhe.Kikwete
aliichagiza jumuiya ya kimataifa kuchangia na kuwekeza katika elimu kwa
mustakabali wa kizazi cha sasa na kijacho. Pamoja naye ni Makamishna
wenzie, Waziri Mkuu wa Norway Erna Solberg na aliyekuwa Waziri Mkuu wa
zamani wa Australia Julia Gillad.IMG_9855 - Copy


Aidha mapato yaliyopatikana kutoka kwenye tamasha hilo yatatumika
kwenye masuala mbalimbali ya kimaendeleo kama Elimu, Miondominu na Afya.global-citizen-festival-2016


Kwenye Tamasha hilo pia wasanii maarufu wa Marekani, Rihanna, Kendrick Lamar, Usher, Demi lovato na Martin Rock walitumbuiza.