Soundcloud

Lipumba akalia kiti chake CUF

Profesa Ibrahim Lipumba aingia ndani ya ofisi za CUF makao makuu jijini Dar es salaam kama mwenyekiti wa chama hicho baada ya barua ya Msajili wa vyama vya siasa kutoa barua ya kumtambua kuwa bado ni mwenyekiti halali wa CUF. Prof-Ibrahim-Lipumba
Akizungumza na waandishi wa habari Jumamosi hii akiwa ofisini kwake Buguruni jijini Dar es salaam, Lipumba amesema huu ndio wakati wake wa kuzungumza na wanachama wake juu ya kukijenga upya cha hicho.
“Sasa hivi mimi nitafanya kazi kama mwenyekiti na kuna mambo yanabidi yarekebishwe ndani ya chama na nitayafanyia marekebisho yanayohitajika. Lakini pia tutafuata katiba na kanuni za chama kuhakikisha nakijenga chama chetu,” alisema Lipumba.
Alipoulizwa kuhusu hali hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro alikiri kupokea barua ya msajili.
Hata hivyo, Mtatiro amesema kwa vyovyote vile msajili wa vyama vya siasa hana mamlaka ya kuingilia maamuzi ya vikao vya chama chochote cha siasa.