http://www.geofreymedia.com/p/wasiliana-nasi.html

Masanja na Mpoki Kimenuka Vibaya

Siku chache tangu m c h e k e s h a j i mwenye jina kubwa Bongo, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ auage ukapera kufuatia ndoa yake ...


Siku chache tangu m c h e k e s h a j i mwenye jina kubwa Bongo, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ auage ukapera kufuatia ndoa yake iliyozua gumzo, nyepesi nyepesi za mjini zinasema kuwa kutoonekana katika shughuli hiyo kwa msanii mwingine, Silvery Mujuni ‘Mpoki’ kunatokana na bifu zito lililopo kati yao, Risasi Mchanganyiko limedokezwa.

Mpoki na Vengu walikuwa ndiyo wasanii pekee wa kundi mahiri la vichekesho la Orijino Komedi ambao hawakutokea katika shughuli hiyo ambayo awali ilianzia katika Kanisa la Miito ya Baraka Kariakoo na baadaye katika Ukumbi wa Prime Rose, Mbezi Beach jijini Dar. Inafahamika kuwa Vengu ana matatizo ya kiafya na hajaonekana hadharani kitambo sasa.


KISIKIE CHANZO
 Chanzo chetu ambacho kiliomba hifadhi ya jina lake, kilisema ilikuwa ni jambo la lazima kwa Mpoki kuwepo katika shughuli hiyo, kwani alikuwa jijini, lakini kuwepo kwa tofauti kati yao, kulisababisha mtangazaji huyo wa redio kwa sasa, kutoonekana kwenye harusi na tafrija ya memba mwenzake huyo, anayetajwa kuwa ndiye mwenye mafanikio zaidi kuliko wote ndani ya kundi lao. “Mimi nawaambieni Masanja na Mpoki kuna kitu. Jiulizeni kwa nini waigizaji wengine wa kundi lao walijitokeza kumsapoti mwenzao kwa kukata mauno kasoro lakini Mpoki hakuhudhuria wakati alikuwa hapahapa mjini akiendelea na mishemishe zake? Fuatilieni, kuna kaukweli,” kilisema chanzo hicho.

RISASI MCHANGANYIKO LAINGIA MZIGONI
Kufuatia madai hayo, gazeti hili liliingia mzigoni kufuatilia ukweli wa jambo hilo na sehemu ya kwanza, ilikuwa ni kwenye mitandao ya kijamii ambako lilihoji kulikoni Orijino Komedi? Katika mtandao mmoja maarufu Bongo, wachangiaji mbalimbali nao walionesha kuhoji sababu za msanii huyo, ambaye pia hujiita Mwarabu wa Dubai, kutoonekana, wakidai kuwepo kwa matatizo kati yao, yanayosababishwa na masilahi. “Ishu siyo Masanja na Mpoki ni Mpoki na Kundi la Orijino Komedi. Kundi linaonekana kama limekufa, hawatoi kazi mpya, kila mtu anaonekana kufanya kazi kivyake na  hawashirikiani katika shughuli za kijamii kama zamani,” aliandika mchangiaji mmoja katika mtandao huo. Mchangiaji mwingine alisema kuwa tatizo linalotokea ni ukweli kuwa Masanja Mkandamizaji, ambaye ni kinda katika sanaa kuliko Mpoki na Joti, amefanikiwa sana kutoka kimaisha kuliko wenzake, jambo linalowafanya waingiwe na kinyongo. Baada ya mitandao hiyo na kuona maoni hayo ya wachangiaji, gazeti hili liliamua kukata mzizi wa fitina kwa kujaribu kuwafikia wasanii hao ili kupata ukweli wao.

HUYU HAPA MASANJA MKANDAMIZAJI
“Mimi na Mpoki ni kama ndugu kaka, hakuna kitu kama hicho, siku ya ndoa yangu alikuwa na mambo yake binafsi, ndiyo maana hakuweza kutokea, lakini wengine walimuwakilisha, kwa hiyo hizo tetesi hazina mashiko kabisa,” alifunguka Masanja na kuongeza; “Madai ya kundi kumomonyoka pia hayana ukweli wowote, Orijino Komedi inaendelea na kazi zake kama kawaida, napenda kuwaambia tu Watanzania kwenye kundi letu kulikuwa na mlango wa kuingilia tu na hakuna wa kutokea, kama mnabisha au mnataka kuamini zaidi basi zungumza na msemaji wa kundi, Seki,” alisema.

MPOKI ASAKWA, AKAUSHA
 Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Mpoki kupitia simu yake ya mkononi, lakini haikupokelewa na alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno, alikataa kusema lolote, badala yake akajibu; “Namba ya Masanja hiyo muulize,” alisema huku akitoa namba ya muigizaji mwenzake huyo. SEKI SASA Kiongozi na msemaji wa kundi hilo, Sekioni David maarufu kama Seki, alisema kundi lao lipo imara ingawa ni muda mrefu hawajatoa kazi. “Wasanii wapo mapumziko na tunatumia muda huu ili kuboresha mikataba yetu ili tutakaporudi, tutakuja na kitu kingine tofauti kabisa.” Kuhusu kutoonekana kwa Mpoki harusini na kwenye sherehe, msemaji huyo ambaye pia ni msanii wa kuigiza sauti za watu, alisema; “Kwa nini humuulizi Vengu, kulikuwa na wawakilishi wake pale mbona huwasemi? Si unafahamu kama Mpoki pia ni MC? Siku hiyo alikuwa na kazi nyingine ndiyo maana hakutokea.”

GEOFREY MEDIA TV

https://www.youtube.com/channel/UCChlD-6iNka8I9kmuuZ9MKw
Name

AFRIKA AFYA AJIRA MPYA All Africa News BIASHARA BREAKING NEWS brudani BUNGENI BURUDANI DUNIANI ELIMU FAHAMU HABARI HABARI VIDEO HABARI ZA HIVI PUNDE HUZUNI IKUFIKIE JOB KENYA KIMATAIFA KITAIFA LIFE STYLE MA0NI HURU MAGARI MAGAZETI MAGUFULI MAISHA YA GHARAMA MAJUU MAKALA MAPENZI MASTAA MATOKEO MATUKIO MICHEZO MIKOANI MIX MOHAMMED ALI MOVIE MUBASHARA NAFASI ZA KAZI NEW AUDIO RELATIONSHIP remix REPORT SIASA SIASA KIMATAIFA SOCIAL MEDIA TAARIFA TANZIA TEKNOLOJIA TUNDU LISSU TUZO UCHOKOZI UK NEWSPAPER UKATILI UTAFITI UTANI WA MAGUFULI VIDEO VIDEO MPYA VIDEO:HISTORIA
false
ltr
item
GEOFREY MEDIA: Masanja na Mpoki Kimenuka Vibaya
Masanja na Mpoki Kimenuka Vibaya
https://3.bp.blogspot.com/-bxZ9wNLLRZk/V8vS7lzfexI/AAAAAAABN00/IAg4nKZqJw8atlO3NDm0M9ZsBbS7BC7TwCLcB/s1600/CIkoB8NUwAAYsA3.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-bxZ9wNLLRZk/V8vS7lzfexI/AAAAAAABN00/IAg4nKZqJw8atlO3NDm0M9ZsBbS7BC7TwCLcB/s72-c/CIkoB8NUwAAYsA3.jpg
GEOFREY MEDIA
http://www.geofreymedia.co.tz/2016/09/masanja-na-mpoki-kimenuka-vibaya.html
http://www.geofreymedia.co.tz/
http://www.geofreymedia.co.tz/
http://www.geofreymedia.co.tz/2016/09/masanja-na-mpoki-kimenuka-vibaya.html
true
3773606987198414401
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy