Soundcloud

Rapper Shawty Lo wa Marekani afariki kwa ajali mbaya ya gariRapper wa Marekani, Carlos “Shawty Lo” Walker, amefariki kwa ajali ya gari iliyotokea Jumatano hii huko Fulton County, Georgia. Alikuwa na miaka 40.
shawty-lo
Meneja wa Shawty Lo, Johnnie Cabbell alitumia akaunti ya Twitter ya rapper huyo kuthibitisha kifo cha rapper huyo.
“My brother has passed; he is no longer here but his spirit, his kind heart and his music will live on,” aliandika Cabbell. “Long live Shawty Lo King of Bankhead.”
“I am so so so devastated that words can not describe how I feel right now,” aliandika Cabbell kwenye Instagram.
“Shawty Lo was not just my artist he was my Brother He was My Friend. I have been Lo MGR for over 10 [years]. He was Loyal and he had my back when no one else did. I could count on him when I had no one else to turn to. We been thru so much together. If you knew Lo, then you know he was genuine. He was Real.”
Kwa mujibu polisi, Walker alikuwa akiendesha gari la Audi na likagonga uzio wa barabara, likagonga miti miwili na kuwaka moto. Amedaiwa kufariki pale pale. Watu wengine wawili waliokuwa kwenye gari hilo walipelekwa hospitali kutibiwa majeraha ya kawaida.