Soundcloud

Saad Lamjarred wa Morocco, ni mwanamuziki mkubwa kuzidi Davido, Wizkid au DiamondKimuziki, Afrika Kaskazini imejitenga na nchi zingine za Afrika, Kusini, Mashariki na Magharibi.


13671749_718743011610699_1136718426_n


Kutokana na hilo, tumejikuta tukishindwa kuwafahamu wasanii wakubwa
wa nchi kama Morocco, Misri, Algeria na kwingine. Mfano, Saad Lamjarred
ni msanii mkubwa wa Morocco, ambaye namba zake zinatisha – ni balaa
kabisa!Kwanza ana followers milioni 3.5 Instagram. Hiyo inafuta kile
tulichokuwa tunaamini kuwa, Davido ndiye mwanamuziki wa Afrika mwenye
followers wengi zaidi kwenye mtandao huo (2.9m) akifuatiwa na Diamond
(2.7m) huku Wizkid akiwa na 2.5m.
Video yake mpya, GHALTANA ilitoka August 25, lakini hadi sasa
imeangaliwa kwa zaidi ya mara milioni 36. Kama hiyo haitoshi, video ya
wimbo wake, LM3ALLEM iliyotoka May 2, 2015 ina zaidi ya views milioni
390.LM3ALLEM uliingia kwenye kitabu cha Guinness World Record kwa kupata
views milioni 100 ndani ya miezi mitatu. Ni video ya kiarabu
iliyotazamwa kuliko zote.13652127_1146218695438772_1391975376_n


Nyimbo zake “Mal Habibi Malou” na “Machi Sahel” zimevutia views milioni 161 na milioni 66 kwenye Youtube hadi sasa.