Soundcloud

Alichokizungumza Rais Magufuli kuhusu mikopo ya wanafunzi vyuo vikuu

Baada ya kuwepo kwa hatua mbalimbali za wanafunzi wa vyuo kudai ongezeko la fedha ya kujikimu na kupatiwa mkopo kwa wanafunzi ambao hawajapatiwa mikopo na baadae Wizara kuahidi kushughulikia suala hilo.
Leo October 21 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Rais Magufuli wakati akihutubia amegusia suala la mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu na kusema Serikali imetenga Sh Bilioni 483 kwa mwaka huu ambapo wanafunzi takribani 93,000 wanaoendelea na masomo na wanafunzi takribani 25,000 watakaoanza masomo watapatiwa mikopo lakini ameweka bayana kuwa mikopo hiyo itatolewa kwa wanafunzi ambao wanatoka kwenye familia masikini.
Aidha Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kurekebisha dosari zilizopo katika mfumo wa utoaji wa mikopo ikiwa ni pamoja na upangaji mbaya wa wanafunzi katika vyuo, kutoa mikopo kwa upendeleo, kutozingatia sifa za mkopaji, kutoa mikopo hewa na kufungua vyuo kabla ya mikopo ya wanafunzi kutolewa na pia amewaonya wanafunzi kujiepusha na vitendo visivyofaa wakati Serikali inarekebisha dosari hizo. Rais Magufuli amesema………
>>>’Vyuo vyote vya elimu ya juu viwe na tarehe moja ya kufungua, ukishafungua kwa haraharaka wakakaa pale kwa mwezi mmoja halafu unawaambia kufanya usajili lazima walipe wakati bodi haijatoa orodha ya majina ya vijana watakaokopeshwa, lazima kuwepo na mawasiliano kati ya bodi ya mikopo, TCU, wizara ya Elimu na wizara ya fedha’
>>>’lengo la serikali si kuleta usumbufu kwa wanafunzi, lakini ni ukweli pia haitatoa mkopo kwa wanafunzi wenye uwezo, mtoto wa Ndalichako naye apate mkopo?, mtoto wa katibu mkuu Kijazi naye apate mkopo? haiwezekani, mkopo huu umelenga kwa ajili ya kutoa watoto maskini lakini nasikia kule kuna upendeleo fulani katika kutoa mkopo sasa hili Waziri na bodi zinazohusike msimamie’;-JPM

SOURCE:MillardAyo.com