Soundcloud

Barakah The Prince: Nay wa Mitego hana akili, ni mp*mbavu, ni rapper anayeungaunga

Barakah The Prince ametema cheche – tena cheche za moto mkali.Baada ya Nay wa Mitego kudai kuwa muimbaji huyo wa ‘Nisamehe’ na Stan Bakora ni watoto na kwamba huenda wanatafuta kiki, ameibuka na kudai kuwa rapper huyo hana akili na mp*mbavu.


“Nay hana akili, yaani Nay wa Mitego ni mp*mbavu tu,” Barakah
alimwambia mtangazaji wa kipindi cha Mdundo Bando cha Lake FM, JR
Junior.
“Yeye ndio anaishi kwa makiki ndio maana mpaka alifungiwa kwa kupiga
madada za watu picha za uchi, sio mwanamuziki mzuri,” alisisitiza msanii
huyo.
“Nay wa Mitego ni rapper anayeungaunga, yaani huwezi kumweka miongoni
kwa rappers wakali Bongo, huwezi kunitajia Nay wa Mitego nikakuambia
kwamba ni rapper mkali. Kwahiyo naye akija akaongea shit about me yaani
nitamshangaa.”


Msikilize zaidi Barakah hapo juu akiporomosha mabomu!