Soundcloud

Hakuna siri tena: Mahusiano ya Young Dee na Amber Lulu hadharani

Ukimwaga mboga wenzio wanamwaga ugali. Ukweli wafahamika baada ya
mara kadhaa rapper Young Dee kukanusha kuwahi kuwa na mahusiano na video
vixen kutoka kwenye kiwanda cha Bongo Fleva, Amber Lulu.
da


Akiongea na U-Heard ya Clouds FM, Amber Lulu amefunguka ukweli kwa
kusema kuwa amekuwa na mahusiano na rapper huyo kwa tangu miaka minne
iliyopita wakati akiwa mkoani Mbeya.
“Marafiki zangu wanajua ni jinsi gani nilivyokuwa naishi naye, mara
ya mwisho alikamatwa na polisi mimi ndio nilienda kumtoa ndugu zake wote
walikataa kwenda, Mimi nimeenda. Matatizo yangu yeye anayafurahia ina
maana. Sikuwa nimefanya vile kwa kuwa alikuwa ni mpenzi wangu ni mtu
ninayemfahamu siku nyingi na ambaye tupo wote,” amesema Amber.