Soundcloud

Izzo Bizness asema hakuna kitacholiyumbisha Kundi la ‘The Amazing’


Mmoja kati ya wasanii wanaounda Kundi la ‘The Amazing’ Izzo Bizness amesema kundi hilo limejipanga kukabiliana na changamoto ambazo zimekuwa zikiyakabili baadhi ya makundi ya muziki nchini.
aa5b76cd-86f7-426c-b923-249e2a0bf723
Rapper huyo ambaye ameshirikiana na muimbaji, Abela kuunda kundi hilo, ameiambia Bongo5 kuwa kabla ya kuunda kundi hilo walikaacha chini na kuangalia namna ambavyo wataweza kukabiliana na matatizo.
“Sisi tumejipanga kupambana na changamoto zote, mpaka kuja au kufikia maamuzi ya kuungana na kuanzisha kundi tayari tumeshasomana tabia, yaani sisi tuna mengi ambayo tuliyaangalia. Kwahiyo naweza sema tupo vizuri tunaomba Mungu atusimamie tu,”
Pia rapa huyo amesema muziki kwa sasa umebadilika na kuwafanya wasanii kuacha kutegemea show pekee.
“Kwa sasa ukifanya muziki mzuri utaona matunda ya muziki wako kwa sababu sasa hivi wasanii hatutegemei shows tu, watu wanapata deal kubwa za kupiga show za mkampuni, endorsement na mambo mengine. Kwahiyo mimi naona kuna mashavu mengi sana kwenye muziki kama ukiandaa kazi nzuri,”