Soundcloud

Katumbi: Nitarejea DR Congo kuwania Urais

Mwanasiasa aliyetangaza nia ya kuwania urais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo , Moise Katumbi, ambaye amekuwa akiishi uhamishoni, amesema atarejea nyumbani.
_91501260_f13ba58a-938f-4c08-b2b1-a864a8ddebda
Katumbi, ambaye alikuwa rafiki wa karibu wa zamani wa Rais Joseph Kabila amekuwa akiishi Ubelgiji. Aliondoka nchini DR Congo mapema mwaka huu baada ya kutuhumiwa kuajiri mamluki kwa lengo la kupindua serikali ya Rais Kabila.
Na baadaye mwezi Juni, alipatikana na hatia ya kuuza nyumba kinyume cha sheria na akahukumiwa kifungo cha miezi 36 jela. Akiongea na BBC akiwa ziarani London, Katumbi amesema: Mimi ni raia wa Congo, nitarejea nyumbani na bado nawania urais. Tuhuma kwamba nilipanga kupindua serikali zinakusudiwa kunizuia.”