Soundcloud

Kimbunga Chaba chaua watu Korea Kusini, chaelekea Japan

Wahudumu wa feri waliokuwa wamerushwa majini na kimbunga hicho wakiokolewa
Watu watano wameuawa na wengine wengi kuachwa bila makao baada ya kimbunga kwa jina Chaba kufika maeneo ya Korea Kusini kikiwa kimeandamana na upepo mkali na mvua.

Miji ya Busan na Ulsan kusini mwa nchi hiyo ndiyo iliyoathiriwa zaidi.
Kisiwa chenye hoteli za kitalii cha Jeju pia kimeathiriwa sana.
Shughuli za uchukuzi, viwanda, shule na uwanja mkuu wa ndege nchini humo zimekwama.
Picha zimeonesha maji ya mafuriko yakiwaa yamejaa barabarani.
Kimbunga hicho kwa sasa kinaelekea Japan ambapo idara ya utabiri wa hali ya hewa huko imetoa tahadhari na kusitisha safari za ndege.
Upepo ulifikia kasi ya 200km/h (124mph), na kung'oa miti Changwon
Barabara nyingi zimefurika maji
Watu wakiokolewa
Magari yaliyokuwa yameharibiwa na kimbunga kisiwani Jeju
Mawimbi yalitangulia upepo mkali ksiiwa cha Jeju
CHANZO:BBCSWAHILI