Soundcloud

MAKONDA AWAJIBU MAWAZIRI WANAOHOJI ANATAFUTA NINI

Mkuu wa mkoa wa Dar Paul Makonda amesema kuna watu wanaohoji wakiwemo mawaziri kuwa anatafuta nini?

Yeye amesema hawezi kujizuia na anawajibu kuwa anatafuta kutimiza kusudi
la Mungu kwenye nafasi aliyopewa, na kingine ni kuwapa heshima waliompa
nafasi aliyonayo

Amesema kuna watu wengi walikuwa wanaongea kuhusu yeye kupewa nafasi ya
ukuu wa mkoa wakati yeye ni mdogo na hataweza lakini licha ya hayo rais
akamuamini na kumteua

Lingine amesema anataka aache alama kuwa kuna mtu alikuwa mkuu wa mkoa wa Dar na akafanya mambo kadhaaAngalia Video