Soundcloud

Video: Bondia afariki dunia baada ya kupokea kichapo ulingoni

Bondia Mike Towell (25) amefariki dunia baada ya kupoteza pambano
lake na Dale Evans kwenye mzunguko wa tano. Pambano hilo lilifanyika
kwenye ukumbi wa St Andrews Sporting Club Alhamisi iliyopita.


Baada ya kupoteza pambano hilo hali yake ilibadilika na kukimbizwa hospitali ambako baadaye alifariki dunia.


Ripoti ya madaktari imeonesha kifo cha Mike kimesababishwa na
kuvujiwa na damu nyingi kwenye ubongo baada ya fuvu lake kupata madhara.

Kabla ya kupoteza pambano hilo bondia huyo aliangushwa mara mbili
kwenye mzunguko wa kwanza kabla ya kuangushwa tena kwa konde zito na
kushindwa kuendelea na pambano.