Soundcloud

CCM inavyoenda wataisoma namba – Rais Magufuli


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, Mhe Dkt. John Pombe Magufuli amesema Chama chake kimekuwa kikiimarika kila siku ndiyo maana kimeanza kukimbiliwa na watu mbalimbali kutoka kwenye vyama vya upinzani.
Rais Magufuli amesema kwa sasa ni mwanzo tu kwani mwaka 2020 Vyama vingine lazima viisome namba kwa kukimbiwa na wanachama wao.
Napenda pia niwashukuru sana wanachama wapya wa UWT, 2,800 sio kitu kidogo napenda niwakaribishe na kuwajulisha kwamba mmefanya uamuzi mzuri, UWT safi, CCM ni chama safi.. Na ni ukweli CCM inavyoenda wataisoma namba tu wale wengine.“amesema Rais Magufuli leo kwenye Mkutano Mkutano Mkuu wa UWT mkoani Dodoma.
Kwa upande mwingine kwenye Mkutano huo Rais Magufuli ambaye ndiye mwenyekiti wa CCM amepokea Wanachama wapya 2,880 akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ambaye alikuwa Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, RC Anna Mghwira.

Post a Comment