Soundcloud

Chanzo cha bifu ya Gurdiola na Mourinho

Jumapili hii wanasema hatumwi mtoto dukani, kila mti atatupia macho yake katika uwanja wa Old Traford ambapo Jose Mourinho atamkaribisha Pep Gurdiola katika mchezo ambao unatajwa kati ya michezo yenye msisimko mkubwa msimu huu.
Wazungu wanasema “Its a war between Genius and Giant” wakimaanisha ni vita baina ya mtu mwenye akili sana na mtu mbabe sana, hii ni kutokana na akili alizonazo Pep Gurdiola na nguvu na kutokukubali kushindwa kwa Jose Mourinho.
Ni kweli Mou na Pep hawaelewani? Iko wazi hawako sawa japo wanapeana mikono ili kuiaminisha jamii wako sawa lakini Pep hayuko sawa na Mou na Mou hayuko sawa na Pep na ndio maana hata mashabiki na wachezaji wa Barca hawampendi Mou kwa sababu ya Pep.
Nini haswa cha ugomvi wao? 1996-2000 Mourinho alikuwa kocha msaidizi wa Barcelona na wakati huo Pep Gurdiola alikuwa kati ya wachezaji wanaoaminiwa sana katika klabu ya Barcelona.
Pep Gurdiola alikuwa kipenzi cha benchi la ufundi na baadhi ya magazeti ya Hispania yanasema alikuwa akitumia mda mwingi na Mourinho kiasi kwamba Mourinho alimpa muda wa ziada Gurdiola.
Mourinho alikuwa akimpa Pep Gurdiola baadhi ya mbinu alizopaswa kufanya uwanjani lakini pia inadaiwa kwamba Mourinho alikuwa akimuandaa Jose kuwa kocha kwa kutokujua kwamba atakuwa tatizo baadaye.
Ugomvi haswa ulitokea wapi? Ilikuwa mwaka 2008, japokuwa mengi yaliongelewa baadaye lakini chanzo haswa cha ugomvi wa wawili hawa ilikuwa mwaka 2008 wakati Barcelona wakitafuta kocha mpya.
Wengi waliamini kwamba Barca watampa ukocha Mourinho kutokana na uzoefu wake ndani ya klabu ya Barcelona lakini vilevile uzoefu wake mkubwa ambao aliupata akiwa na Wacatalunya.
Mezani kulikuwa na majina mawili Pep Gurdiola na Jose Mourinho lakini Mou alianza kupigwa vita kutokana na aina yake ya anavyoamini mpira unapaswa kucheza na wengi wakasema hana mtazamo unaoendana na Barcelona.
Johan Cruyff gwiji wa zamani wa Barcelona aliamua kucheza kamali na kumpa ukocha mtu ambaye hakuwa na uzoefu mkubwa na soka  ni Pep Gurdiola na kuanzia siku hiyo inadaiwa kwamba wawili hawa ugomvi ukaanza na kilichotokea kuhusu uhusiano wao ndio kinachoendelea hadi sasa.
CHANZO: Shaffi Dauda

Post a Comment