Soundcloud

Rais Magufuli alitaka Jeshi la Magereza kutumia wafungwa kwa uzalishaji


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John P. Magufuli leo ametia saini nyaraka za msamaha kwa wafungwa 61 waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa ambapo ametumia fursa hiyo pia kulitaka jeshi la Magereza kuwatumia wafungwa kwa uzalishaji.
Rais Dkt. John Magufuli akitia saini nyaraka za msamaha alioutoa kwa wafungwa 61 waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa na wawili Nguza Viking (Babu Seya) na Johnson Nguza (Papii Kocha) waliohukumiwa kifungo cha maisha jela.

Rais Magufuli ametia saini nyaraka hizo leo Jumapili Desemba 10,2017 Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma, ikiwa ni siku moja tangu atangaze Msamaha kwa wafungwa akiwemo Msanii wa muziki wa dansi,Nguza vikingi na Mtoto wake Johnson  Nguza (Papii Kocha)Post a Comment