Soundcloud

Easter Bulaya na Halima Mdee wakoshwa na Vanessa Mdee


Wakati albamu mpya ya Vanessa Mdee  ‘Money Mondays’ ikiendelea kufanya vizuri mtaani, msanii huyo amefunguka kupokea pongezi kutoka kwa watu mbali mbali maarufu.
Muimbaji huyo ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa miongoni mwa waliompongeza ni Mbunge wa Bunda, Easter Bulaya na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee.
“Huwezi amini nimepigiwa simu na Easter Bulaya jana akaniambia mamii wimbo wako unaitwa Bambino ambao nimemshirikisha siitoi muda wote nacheza, akasema niko na Halima Mdee akasema sisi si wapare, so nafurahi napata support kutoka kwa watu wengi,” amesema.
Albumu ya Vanessa Mdee  ‘Money Mondays’ iliyoingia mtaani Junuary 20 mwaka huu ina nyimbo zipatazo 17.

Post a Comment