Soundcloud

ETO’O AZINDUA MASHINDANO YA CASTLE AFRICA 5-A-SIDE, TANZANIA KUSHIRIKI

Maestro (kushoto), Ivo Mapunda na mwenzao.

Legendari WA soka kutoka nchini Cameroon, Samuel Eto’o, amefungua mashindano ya Castle Africa 5-a-side mjini Johannesburg nchini Afrika Kusini juzi ALhamisi ambapo nchi sita zitashiriki ikiwa ni pamoja na Afrika Kusini, Lesotho, Tanzania, Swaziland, Zambia na Zimbabwe.
Mabalozi wa Castle wakiwa na Samuel Eto’o (katikati).

Mashindano hayo ambayo yataanza Februari 1 mwaka huu hadi Mei mwaka huu yataanza na mashindano ya ndani kwa kila nchi ambapo kwa Tanzania mkoa wa Dar es Salaam washiriki watakuwa kila wilaya zote tano ambazo kila wilaya itatoa timu moja zitakazochuana kupata mshindi mmoja ambaye atakwenda Zambia kwa ajili ya fainali.

Timu Mshindi wa fainali hiyo atapata fursa ya kupelekwa nchini Russia kushuhudia fainali za Kombe la dunia zitakazofanyika mwaka huu.
Eto’o ambaye amewahi kucheza vilabu vikubwa duniani kama Real Madrid, Barcelona na Inter Milan na kwa sasa yupo Uturuki katika klabu ya Antalyaspor alikuwa ndiye mgeni wa heshima wakati wa uzinduzi huo.
Mbali na Eto’oo, mabalozi wengine wa Castle katika michuano hiyo ni Lehlohonolo Seema(Lesotho), Tinashe Nengomasha (Zimbabwe), Christopher Katongo (Zambia), Siza Dlamini (Swaziland) na Ivo Mapunda (Tanzania).

Post a Comment