Soundcloud

Man United hawana mpango na Ronaldo, Sanchez anawatosha


Klabu ya soka ya Manchester United haina mpango wa kumsajili tena mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo ambaye amekuwa na wakati mgumu Real Madrid.
Kwa mujibu wa gazeti la michezo la Marca kutoa Hispania limesema hilo kutokana na Man United tayari wanakaribia kumsaini Alexis Sanchez kutoka Arsenal ambaye anatarajiwa kuvaa jezi namba saba katika timu hiyo ambapo jezi hiyo iliwahi kuvaliwa na Ronaldo wakati akichezea timu hiyo.
Inadaiwa kuwa sababu kubwa ya Ronaldo kutokuwa na furaha ndani ya Madrid ni kutokana Rais wa Madrid, Florentino Perez kuvunja ahadi ya kumuongeza mshahara wake ambapo kwa sasa analipwa paundi milioni 21 kwa mwaka.

Post a Comment