http://www.geofreymedia.com/p/wasiliana-nasi.html

Mh. Lissu apelekwa Ubelgiji kwa matibabu zaidi

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu ametoka Hospitali ya Nairobi nchini Kenya leo Jumamosi asubuhi kwenda nchini Ubelgij...


Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu ametoka Hospitali ya Nairobi nchini Kenya leo Jumamosi asubuhi kwenda nchini Ubelgiji kwa matibabu zaidi ya kuurejesha mwili wake katika hali yake ya kawaida.
Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanzania (TLS) ataondoka saa 2.30 asubuhi ya leo Jumamosi na Ndege ya Shirika la Kenya akiambatana na mke wake, Alicia.
Lissu ametoka hospitalini hapo ikiwa baada ya matibabu aliyoyapata tangu Septemba 7 mwaka jana baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana kwenye makazi yake Dodoma.
Mwanasiasa huyo amesindikizwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta na watoto wake pacha, Augustino na Edward, ndugu zake, viongozi na wanachama wa Chadema.
“Nawashukuru sana madaktari wa hapa Nairobi na wale wa Dodoma wakiongozwa na Katibu Mkuu (wa wizara ya afya Profesa Mpoki Ulisubisya waliookoa maisha yangu,” amesema Lissu kabla ya kupandishwa gari la wagonjwa
“Nakwenda Ubelgiji kwa matibabu, nikirudi mapambano yanaendelea, nawashukuruni nyote mlioniombea, nawashukuru Wakenya na serikali yao ambao kwa miezi minne nikiwa hapa walinipa ulinzi wakati wote.”
Akizungumza kwa msisitizo mbele ya wabunge na wanachama wa Chadema waliokuwapo amesema “Chapeni kazi, mimi nitarudi kuendeleza mapambano haya.”
Kuhusu gharama, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji amesema gharama za safari na matibabu zimegharamikiwa na Chadema na TLS.
Wakati baadhi ya waliokuwapo hospitalini kumsindikiza Lissu uwanja wa ndege ni kaka yake Alute Mghwai, mdogo wake, Vinceti Mghwai na ndugu wengine.
Pia, Dk Mashinji, Naibu Makatibu Wakuu, John Mnyika (Bara), Salum Mwalimu (Zanzibar).
Wengine walikuwapo ni wabuge wa Chadema, Susan Kiwanga (Mlimba) na Godbless Lema(Arusha Mjini), John Heche (Tarime Vijijini), Rose Kamili (Viti Maalum), Anna Gideria (Viti Maalum).
Kwa niaba ya familia, Alute amesema “Tunamwomba Mungu ajalie huko anakokwenda akapate matibabu, kwani alivyokuja hapa sivyo anavyoondoka na tunawashukuru wananchi wa Tanzania na Kenya kwa ushirikiano wao.”
Chanzo; Mwananchi

COMMENTS

GEOFREY MEDIA TV

https://www.youtube.com/channel/UCChlD-6iNka8I9kmuuZ9MKw
Name

AFRIKA AFYA AJIRA MPYA All Africa News BIASHARA BREAKING NEWS brudani BUNGENI BURUDANI DUNIANI ELIMU FAHAMU HABARI HABARI VIDEO HABARI ZA HIVI PUNDE HUZUNI IKUFIKIE JOB KENYA KIMATAIFA KITAIFA LIFE STYLE MA0NI HURU MAGARI MAGAZETI MAGUFULI MAISHA YA GHARAMA MAJUU MAKALA MAPENZI MASTAA MATOKEO MATUKIO MICHEZO MIKOANI MIX MOHAMMED ALI MOVIE MUBASHARA NAFASI ZA KAZI NEW AUDIO RELATIONSHIP remix REPORT SIASA SIASA KIMATAIFA SOCIAL MEDIA TAARIFA TANZIA TEKNOLOJIA TUNDU LISSU TUZO UCHOKOZI UK NEWSPAPER UKATILI UTAFITI UTANI WA MAGUFULI VIDEO VIDEO MPYA VIDEO:HISTORIA
false
ltr
item
GEOFREY MEDIA: Mh. Lissu apelekwa Ubelgiji kwa matibabu zaidi
Mh. Lissu apelekwa Ubelgiji kwa matibabu zaidi
https://1.bp.blogspot.com/-usVxnh16zqk/WlDHRo0qoYI/AAAAAAAAD_U/a90Z9i0dUcU_ZDCCDC6q1DxjzI8_sgUggCLcBGAs/s400/55a52e5c-b5ce-4290-8a52-2d570a3e955e.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-usVxnh16zqk/WlDHRo0qoYI/AAAAAAAAD_U/a90Z9i0dUcU_ZDCCDC6q1DxjzI8_sgUggCLcBGAs/s72-c/55a52e5c-b5ce-4290-8a52-2d570a3e955e.jpg
GEOFREY MEDIA
http://www.geofreymedia.co.tz/2018/01/mh-lissu-apelekwa-ubelgiji-kwa-matibabu.html
http://www.geofreymedia.co.tz/
http://www.geofreymedia.co.tz/
http://www.geofreymedia.co.tz/2018/01/mh-lissu-apelekwa-ubelgiji-kwa-matibabu.html
true
3773606987198414401
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy