Soundcloud

MSHAHARA WA SANCHEZ KUFURU MAN UNITED

STAA wa Arsenal, Alexis Sanchez anatarajiwa kusaini mkataba wa kujiunga na Manchester United muda wowote kuanzia sasa, inaelezwa kuwa atakuwa akilipwa mshahara wa pauni 18m kwa mwaka.

Ikiwa atasaini mkataba huo, atakuwa akilipwa pauni 350,000 kwa wiki na kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi klabuni hapo kwa sasa licha ya kuwa hatavunja rekodi ya kuwa mchezaji ambaye amewahi kulipwa mshahara mkubwa ndani ya United.

Zlatan Ibrahimovic ndiye aliyekuwa akilipwa mshahara mkubwa msimu uliopita, ambapo alikuwa akilipwa pauni 367,640 kwa wiki.

Ili kukamilika kwa dili hilo la uhamisho wa Sanchez inaelezwa kuwa inasubiriwa Henrikh Mkhitaryan akubali kuhusika kwa kuwa Arsenal inamtaka mchezaji huyo ambaye analipwa pauni 140,000 kwa wiki.
Sanchez akikamilisha dili atakuwa juu ya kiungo mwenye thamani kubwa kuliko wote ndani ya United, Paul Pogba ambaye analipwa pauni 260,000 kwa wiki.

Msimu uliopita Pogba alikuwa akilipwa pauni 165,000 lakini mshahara uliongezeka hadi kuwa pauni 200,000 baada ya kushinda Europa League, lakini kutokana na kukua kwa jina lake kibiashara, napo kuna nyongeza ya fedha ambayo inafanya ifike pauni 260,000. Mbali na hapo kuna posho ambayo inaweza kuwa chini ya pauni 3.5m kwa mwaka.

Orodha kamili ya wachezaji wanaolipwa mishahara mikubwa United kwa wiki ikiwa Sanchez atatua, itakuwa hivi (alama ya £ ni pauni):
MISHAHARA MIKUBWA MAN UNITED
  1. Alexis Sanchez £350,000
  2. Paul Pogba £260,000
  3. Romelu Lukaku £220,000
  4. David de Gea £200,000
  5. Ibrahimovic £150,000
  6. Juan Mata £145,000
  7. Nemanja Matic £140,000
  8. Mkhitaryan £140,000
  9. Fellaini £120,000
  10. Chris Smalling £120,000

Post a Comment