Soundcloud

Rama Dee kufungua mwaka 2018 na ‘Furaha Yetu


Mkali wa R&B Bongo na mshindi wa tuzo mbalimbali za Muziki, Rama Dee ameamua kufungua mwaka 2018 kwa kutaka kuachia ngoma yake mpya iliyo na staili ya twist ambayo italeta utofauti katika kiwanda cha burudani.
Akiongea na Bongo5, Mkali huyo amesema Ijumaa ya wiki hii anatarajia kuachia ngoma yake hiyo iitwayo ‘Furaha Yetu’.
“Idea ya wimbo wa “Furaha Yetu” ilikuja baada ya kuona watu wengi kwenye mahusiano hawana furaha, si kwamba hawapendani no ila hawajui kama wanaishi kwa furaha kwa kuangalia na kuamini vitu vilivyo mbele ya camera”. ameiambia Bongo5.
Amesema “Pia kutokana na experience ya kuzungukwa na marafiki wanaopenda kuchukia kila kitu unachofanya, nako kulifanya wazo la wimbo huo kuibuka , Lakini pia, niligundua marafiki wengi hawana furaha wana-hate kila kitu kizuri wakifanyacho watu wengine, hawajiamini, hawakubali kuwa wapo kwenye ulimwengu wa furaha”.
“Marehemu Mama yangu alipenda sana muziki wa aina hii (twist), pia niliwahi kumwambia siku moja hii style nitaiweka kiujana ili iendelee kupendwa”. Amesisitiza Rama Dee.
Wimbo huo umenyika katika studio za ‘Hometown studio’,  huku akihusikia asilimia kubwa kuuandaa kwa kushirikiana na Elly Da Bway. Hata hivyo mkali huyo anaamini wimbo huu sio kwaajili ya kucheza tu, bali ni maalum kwa kuwakumbusha watu kuwa maisha ni mafupi na wanahitaji kuishi kwa furaha.

Post a Comment