Soundcloud

Sugu arudishwa rumande


Mbunge wa Mbeya mjini, Mhe. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ leo Ijumaa Januari 19, 2018 amerudishwa rumande baada ya kukosa dhamana ya kesi yake inayomkabili ya maneno ya uchochezi.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Mbeya, Michael Mteite amesema sababu ya kumnyima dhamana mshtakiwa Sugu na mwenzake Emmanuel Masonga ni hofu ya mshtakiwa kutohudhuria mahakamani hapo mara kwa mara ile hali Hakimu anataka kesi hiyo iishe mapema.
Mfululizo wa kusikiliza kesi hiyo utaendelea Jumatatu ya tarehe 22. 01.2018.

Post a Comment