Soundcloud

The Weeknd avunja mkataba H&M baada ya ubaguzi


 Msanii wa muziki na mtayarishaji wa muziki, The Weeknd ameamua kukatisha mkataba wake na kampuni H&M iliyokuwa ikimsimamia masuala ya mavazi.
The Weeknd mwenye makazi yake nchini Marekani, ameamua kukatisha mkataba huo kufuatia picha inayosambaa mtandaoni ikimuonyesha mtoto mwenye asili ya mtu mweusi akiwa amevalia T-Shirt iliyoandika maneno ya kiudhalilishaji yakisomeka ‘ Coolest Monker in the Jungle’.
Kufuatia hatua hiyo Abel Makkonen Tesfaye a.k.a The Weeknd ametumia ukurasa wa mtandao wa Twitter kulaani tukio hilo la udhalilishaji na kudai kuto fanya kazi na kampuni hiyo.
 Picha za kijana huyo zilianza kuzagaa siku ya jana mitandaoni huku mastaa kama T.I, P.Diddy, Floyd Joy Mayweather na wengineo wakilani kitendo hicho.

Post a Comment