Soundcloud

‘VISU’ VITANO VIKALI AFRIKA

LUPITA N’YONGO
UKIACHILIA suala zima la rangi ya ngozi na shepu, wanawake wengi wa Afrika wamejaliwa uzuri. Kwa mujibu wa jarida maarufu duniani la Style Craze limekuanikia mademu ‘visu’ vitano vikali kutoka Afrika kwa mwisho wa mwaka 2017;

• LUPITA N’YONGO Bidada huyu ambaye ni muigizaji, direkta wa filamu na muziki na pia mwanamitindo, amezaliwa Machi 1, 1983 nchini Mexico na kukulia nchini Kenya. Lipita amekuwa miongoni mwa visu vinavyowavutia wengi kutokana na muonekano wake (rangi ya ngozi nyeusi) na makampuni mengi kufanya naye kazi kupitia filamu na mitindo.
FATIMA SIAD
FATIMA SIAD Ni kisu cha Afrika kilichozaliwa Desemba 17, 1986, Mogadishu, Somalia kikijikita zaidi katika mitindo. Fatima ambaye ni chotara f’lan kutokana na mama yake kuwa Msomali na baba Muethiopia amekuwa akivutia wengi kutokana na muonekano wake wa sura hadi umbo na kumpelekea kupata dili la mitindo katika Kampuni ya IMG ikimpa  mashavu New York, Paris, Milan na sehemu nyingine kibao.
FREEMA AGYEMAN 
•FREEMA AGYEMAN Freema ni mwanamitindo, muigizaji na mwanamuziki aliyezaliwa Machi 20, 1979 London, Uingereza. Ni miongoni mwa visu Afrika kutokana na muonekano wake wa ngozi na sura huku naye akiwa chotara f’lan kutokana na mama kuwa na asili ya Iran na baba Ghana. Freema anajulikana zaidi kwenye Tamthilia ya Doctor Who akiigiza kama Martha Jones.
AZIE TESFAI 
•AZIE TESFAI Kisu hiki kilizaliwa Desemba 20, Los Angeles, Marekani. Azie ni muigizaji aliyehama nchi yao na kuingia Uingereza. Ni mchanganyiko mwenye asili ya Ethiopia na Eritrea ambapo muonekano wake umempa dili katika Muvi ya Jane the Virgin.
LIYA KEBEDE
•LIYA KEBEDE Amezaliwa Machi 1, 1978 huko Addis Ababa, Ethiopia akiwa kama mwanamitindo. Muonekano wake umemfanya kuhama Ethiopia kwenda kuishi Ufaransa. Kwa sasa ni mwanamitindo aliyenasa makampuni mengi kama vile Yves SaintLaurent, Gap na Victoria’s Secret.

Post a Comment