Soundcloud

KAMPENI MPYA YA JIONGEZE NA M-PESA, SHINDA NA SPORTPESA YAZINDULIWA


KAMPUNI ya michezo ya kubashiri nchini, SportPesa Tanzania kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania jana imezindua promosheni kubwa inayojulikana kama Jiongeze na M-Pesa, Shinda na SportPesa.

Uzinduzi huo ulifanyika jana asubuhi kwenye viwanja wa Mbagala Zakhemjijini Dar es Salaam ambao wateja wanaotumia mtandao wa Vodacom kupitia M-Pesa watapata nafasi ya kushiriki kwenye promosheni hiyo na kujishindia bajaji mpya za aina ya TVS King Deluxe.

Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye ufunguzi wa promosheni hiyo, Meneja Uhusiano wa SportPesa, Sabrina Msuya alisema “Hii ni nafasi nzuri kwetu na wateja wa Vodacom kushiriki kwenye promosheni hii kwa kucheza na SportPesa ili kujishindia bajaji mpya kabisa.

“Huu utakuwa muendeleo wa promosheni ya Shinda na SportPesa iliyomalizika hivi karibuni ambapo bajaji 100 aina ya TVS King zilitolewa kwa washindi kutoka kila kona ya Tanzania huku Mkoa wa Dar es Salaam ukiibuka kidedea kwa kutoa washindi wengi ikifuatiwa na mikoa ya Mwanza, Njombe, Arusha pamoja na Mtwara,”alisema Msuya.

Msuya alisema, ili kushiriki kwenye ptomosheni hii mpya, wateja wa Vodacom wanatakiwa kutuma neno GAME kwenda namba 15888 kujisajili na SportPesa kupitia M-Pesa na kuweka ubashiri ili wajiongezee nafasi ya kushinda.

“Promosheni yetu imeanza rasmi leo (jana) ambapo droo za kuwapata washindi zitachezeshwa kila siku za Jumatatu na Alhamisi ambapo tutarajia kuwa na washindi 20 baada ya wiki kumi za promosheni kumalizika, hivyo napenda kuwahimiza Watanzania wote kushiriki katika promosheni hii ili waweze kuinua na kukuza vipato vyao kupitia bajaji,”alisema Msuya.

Kwa upande wa Meneja Masoko wa Vodacom Tanzania, Noel Mazoya alisema kuwa “Vodacom imeshiriki katika promosheni hii ikiwa ni muendelezo wa dhamira yake ya kurajisisha maisha ya Watanzania kupitia huduma za fedha za kidigitali.

Post a Comment