http://www.geofreymedia.com/p/wasiliana-nasi.html

Mozey Radio:Nyota iliyong'ara kwa Miaka 10 na kuzima Ghafla

Radio Moses Nakintije Ssekibogo radio kama wengi tunavyomfahamu alizaliwa  25 January 1985 huko Busoga Uganda na kuanza shughuli za mu...

Radio
Moses Nakintije Ssekibogo radio kama wengi tunavyomfahamu alizaliwa 25 January 1985 huko Busoga Uganda na kuanza shughuli za muziki mnamo mwaka 2008 wakiunda kundi la muziki liitwalo Goodlyfe akiwa na mdogo wa  Jose Chamelione aitwaye  Weasel.

Radio aliachia wimbo wake wa kwanza kama  Solo artist, ulioitwa  "Sweet Lady", kipindi akiwa katika lebo ya muziki ya Leone Island iliyoko chini ya Jose Chameleone. Baadae akaanza kuimba akiwa na Weasal chini ya Chameleone.

Kufuatia kutoelewana kati ya Jose Chameleone na wawili hao, Radio na Weasal waliamua kuachana na Chameleone na kuamua kuunda kundi lao la GoodLyfe na kufanikiwa sana katika muziki Afrika Mashariki.

Radio & Weasal
Radio amewahi amewahi kuoa mwanamuziki mwenzake aitwae Lilian na kuzaa naye mtoto mmoja na baadaye kuachana naye na kuoa wanawake tofauti tofauti.


Radio atakumbukwa kwa sauti yake ya kipekee katika Muziki was Afrika mashariki akiwa katika kundi la Goodlyfe pamoja na Rafiki yake kipenzi Weasal ambapo waliwahi kutamba na Nyimbo kama Zuwena, Fire & butter, Tambula Nange, Let Dem Know, na nyinginezo nyingi.

Pia Radio mewahi kufanya Kolabo na msanii Rabadaba katika ngoma iliyofanya vizuri sana iliyoitwa Ability akiwa na Weasal iliyotengenezwa na Jose.
Mbali na Rabadaba Radio ameshafanya kazi na Wizkid katika wimbo ulioitwa Don't Cry. Tazama hapo chini....


Mbali na Wizkid, Msanii Kiwango A tokea Tanzania, Vanessa Mdee, naye amewashirikisha Radio na Weasal.
Radio akiwa Stuo na Msanii wa Tanzania,Vanessa Mdee

Radio pia amekuwa akiripotiwa na media mbalimbali za nchini Uganda kugombana na watu mbalimbali ikiwemo mwaka jana ambapo aliripotiwa kuvunja Kompyuta mpakato ya DJ Momoja aliyekataa Kupiga ngoma iliyokuwa ikimuenzi Ivan Semwanga ambaye naye ni marehemu kwa sasa.
Radio akiwa chini ya Ulinzi wa Polisi baada ya kumshambulia Dj,katika klabu moja ya usiku nchini Uganda
22 January mwaka 2018 Radio aliumia vibaya baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana katika ugomvi uliotokea katika Club moja Mjini Entebe nchini Uganda na kumuacha na majeraha makubwa ikiwemo kuumia fuvu lakichwa sehemu ya nyuma na majeraha mengine Shingoni.

Baada ya shambulio hilo alikimbizwa hospitali na alifanyiwa upasuajibkuokoa maisha yake na haliyake iliendelea vizuri baada ya kutolewa ICU ambapo alikuwa akitumia mashine kupumua.....Siku ya Jumamosi alizidiwa na kurudishwa ICU .

Jeneza lenye mwili wa Radio
Mapema leo February 1 mwaka 2018, Madaktari kutoka Case Clinic in Kampala walitangaza kuwa Msanii Radioamefariki majira ya saa 7 kamili Asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki.
Simanzi vilio vilitawala katika maeneo mbalimbali ya Uganda wengi wakiwa hawaamini kilichotokea.
Jeneza lenye mwili wa Radio
Wasanii mbalimbali tokea Afrika Mashariki kama vile Navio,Professa J, Diamond Platnumz na wengine wengi wameungana na waganda na familia ya Radio kumlilia kwa namna yao.

NAVIO:


DAIMOND PLATNUMZ


A post shared by Chibu Dangote (@diamondplatnumz) on

VANESSA MDEE:PROFESA JAY:Naye Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museven ameeleza kusikitishwa na kifo cha Mwanamuziki huyo ambapo jana alitoa takribani Shilingi Milioni 30 kwa feza za Tanzania kwa ajili ya matibabu.


Mseven amlilia Radio
HIZI NI HITS 35 KALI ZA RADIO & WEASAL
1. Don’t cry– Radio & Weasle ft Wizkid
2. Nyambula – Radio & Weasle
3. Gutamiza – Radio & Weasle
4. Hellena – Radio & Weasle ft Lutalo
5. Tukikole Neera – Radio & Weasle
6. Ability – Radio & Weasle ft Rabadaba
7. Magnetic – Radio & Weasle
8. Bread & Butter – Radio & Weasle
9. Nakudata – Radio & Weasle
10. Obudde – Radio & Weasle
11. Ntunga – Radio & Weasle
12. Talk & Talk – Radio & Weasle
13. Kuku – Radio & Weasle
14. Bwondekawo – Radio & Weasle
15. Zino enaku – Radio & Weasle
16. Juicy juicy - Radio & Weasle
17. Ekyaama - Radio & Weasle
18. Nakutamani - Radio & Weasle
19. Vuvuzela - Radio & Weasle
20. Amaaso - Radio & Weasle
21. Can't let you go - Radio & Weasle
22. Omwana wa Bandi  - Radio & Weasle
23. Byagana -  Radio & Weasle
24. Numba emu - Radio & Weasle
25. Get Love -  Radio & Weasle ft WizKid
26. Tompona  - Radio & Weasle ft Leyila
27. Nkwetaga  - Radio & Weasle
28. Breath Away  - Radio & Weasle
29. Zuena  - Radio & Weasle
30. Ole  - Radio & Weasle
31. Potential - Radio & Weasle
32. Sitani - Radio & Weasle
33. Nyumbani - Radio & Weasle
34. Sweat Lady - Mozey Radio

35. Lwaki Onumya -Radio & Weasle
COMMENTS

GEOFREY MEDIA TV

https://www.youtube.com/channel/UCChlD-6iNka8I9kmuuZ9MKw
Name

AFRIKA AFYA AJIRA MPYA All Africa News BIASHARA BREAKING NEWS brudani BUNGENI BURUDANI DUNIANI ELIMU FAHAMU HABARI HABARI VIDEO HABARI ZA HIVI PUNDE HUZUNI IKUFIKIE JOB KENYA KIMATAIFA KITAIFA LIFE STYLE MA0NI HURU MAGARI MAGAZETI MAGUFULI MAISHA YA GHARAMA MAJUU MAKALA MAPENZI MASTAA MATOKEO MATUKIO MICHEZO MIKOANI MIX MOHAMMED ALI MOVIE MUBASHARA NAFASI ZA KAZI NEW AUDIO RELATIONSHIP remix REPORT SIASA SIASA KIMATAIFA SOCIAL MEDIA TAARIFA TANZIA TEKNOLOJIA TUNDU LISSU TUZO UCHOKOZI UK NEWSPAPER UKATILI UTAFITI UTANI WA MAGUFULI VIDEO VIDEO MPYA VIDEO:HISTORIA
false
ltr
item
GEOFREY MEDIA: Mozey Radio:Nyota iliyong'ara kwa Miaka 10 na kuzima Ghafla
Mozey Radio:Nyota iliyong'ara kwa Miaka 10 na kuzima Ghafla
https://4.bp.blogspot.com/-lf4Xe9FiVys/WnM8POF6hAI/AAAAAAAAEWg/wSEWeMV_PqAAnZV-xAp-Eoyo5yIelFr5wCLcBGAs/s400/radio-450x270.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-lf4Xe9FiVys/WnM8POF6hAI/AAAAAAAAEWg/wSEWeMV_PqAAnZV-xAp-Eoyo5yIelFr5wCLcBGAs/s72-c/radio-450x270.jpg
GEOFREY MEDIA
http://www.geofreymedia.co.tz/2018/02/mozey-radionyota-iliyongara-kwa-miaka.html
http://www.geofreymedia.co.tz/
http://www.geofreymedia.co.tz/
http://www.geofreymedia.co.tz/2018/02/mozey-radionyota-iliyongara-kwa-miaka.html
true
3773606987198414401
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy