Soundcloud

Riyad Mahrez kurejea mazoezini Leicester City


Riyad Mahrez anatarajiwa kurejea mazoezini hii leo siku ya Ijumaa ikiwa ni maamuzi yake binafsi na tayari kuisaidia Leicester City itakapo shuka dimbani kuivaa Manchester City siku ya Jumamosi.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Algeria hajafanya mazoezi na klabu hiyo tangu kufeli kwa uhamisho wake wa kujiunga na City wakati wa dirisha la usajili la mwezi Januari.
Meneja wa Leicester Claude Puel kupitia mkutano wake na waandishi wa habari hapo jana siku ya Alhamisi amesema kuwa Mahrez huwenda akaukosa mchezo huo ingawa bado haija fahamika rasmi.

Post a Comment