http://www.geofreymedia.com/p/wasiliana-nasi.html

Wananchi wa Wilaya ya Kwimba Wamkataa Mkuu wa Wilaya Hiyo Mbele ya Waziri Mkuu

Wananchi wa wilaya ya Kwimba mkoani hapa wamemuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuondoka na mkuu wa wilaya hiyo Mtemi Msafiri kwa madai y...


Wananchi wa wilaya ya Kwimba mkoani hapa wamemuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuondoka na mkuu wa wilaya hiyo Mtemi Msafiri kwa madai ya kutoridhishwa na utendaji wake.

Taarifa iliyotolewa leo Februari 16, 2018 na ofisi ya waziri mkuu imeeleza kuwa wananchi hao wametoa kauli hiyo baada ya kuzuia msafara wa Majaliwa alipowasili katika ofisi za Halmashauri ya wilaya Kwimba kwa ajili ya kuzungumza na watumishi, akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza.

Wananchi hao walimkataa mkuu huyo wa wilaya kupitia ujumbe wa mabango 17, Majaliwa kuwataka wananchi hao kuwa watulivu wakati Serikali inafanyia kazi malalamiko yao.

Wananchi hao wamedai Msafiri anatabia ya kuamrisha polisi wawakamate kwa kisingizio cha uzururaji na kisha wanawekwa mahabusu, kisha kutolewa na kupelekwa  kulima kwenye shamba lake.Waziri Mkuu amesema Serikali inahitaji kila mtumishi atambue majukumu yake na ayatekeleze. “Hakuna atakayeonewa, haki zenu zote tunazitekeleza nanyi mnatakiwa kutenda haki kwa kuwatumikia wananchi.”

Hata hivyo, Majaliwa amemtaka mkuu huyo wa wilaya,  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kwimba, Pendo Malebeja na wakuu wote wa Idara wajitathmini kama kweli wanatekeleza majukumu yao ipasavyo na kuwatumikia wananchi.

“Mkurugenzi katika kipindi chako chote cha utendaji kuanzia mwaka 2013 hadi leo, fedha nyingi za Serikali zilizoletwa Kwimba zimepotea na hazijulikani zilipo huku miradi mingi bado haijakamilika na muda wote huo Halmashauri imekuwa inapata hati chafu,” amesema Majaliwa.

COMMENTS

GEOFREY MEDIA TV

https://www.youtube.com/channel/UCChlD-6iNka8I9kmuuZ9MKw
Name

AFRIKA AFYA AJIRA MPYA All Africa News BIASHARA BREAKING NEWS brudani BUNGENI BURUDANI DUNIANI ELIMU FAHAMU HABARI HABARI VIDEO HABARI ZA HIVI PUNDE HUZUNI IKUFIKIE JOB KENYA KIMATAIFA KITAIFA LIFE STYLE MA0NI HURU MAGARI MAGAZETI MAGUFULI MAISHA YA GHARAMA MAJUU MAKALA MAPENZI MASTAA MATOKEO MATUKIO MICHEZO MIKOANI MIX MOHAMMED ALI MOVIE MUBASHARA NAFASI ZA KAZI NEW AUDIO RELATIONSHIP remix REPORT SIASA SIASA KIMATAIFA SOCIAL MEDIA TAARIFA TANZIA TEKNOLOJIA TUNDU LISSU TUZO UCHOKOZI UK NEWSPAPER UKATILI UTAFITI UTANI WA MAGUFULI VIDEO VIDEO MPYA VIDEO:HISTORIA
false
ltr
item
GEOFREY MEDIA: Wananchi wa Wilaya ya Kwimba Wamkataa Mkuu wa Wilaya Hiyo Mbele ya Waziri Mkuu
Wananchi wa Wilaya ya Kwimba Wamkataa Mkuu wa Wilaya Hiyo Mbele ya Waziri Mkuu
https://3.bp.blogspot.com/-21XuKCBlr-8/WodAK_xs6NI/AAAAAAAAEhg/Vbkwzkxw_BQa1t8h_Q3Mu2l0jfa5ALCCACLcBGAs/s400/pm%252B3.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-21XuKCBlr-8/WodAK_xs6NI/AAAAAAAAEhg/Vbkwzkxw_BQa1t8h_Q3Mu2l0jfa5ALCCACLcBGAs/s72-c/pm%252B3.jpg
GEOFREY MEDIA
http://www.geofreymedia.co.tz/2018/02/wananchi-wa-wilaya-ya-kwimba-wamkataa.html
http://www.geofreymedia.co.tz/
http://www.geofreymedia.co.tz/
http://www.geofreymedia.co.tz/2018/02/wananchi-wa-wilaya-ya-kwimba-wamkataa.html
true
3773606987198414401
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy