http://www.geofreymedia.com/p/wasiliana-nasi.html

Ahed Tamimi: Binti Mpalestina aliyemzaba kofi mwanajeshi wa Israel afungwa jela

Binti mmoja wa Kipalestina aliyekamatwa baada ya kumchapa kofi mwanajeshi wa Israel amekiri kosa na atatumikia kifungo cha miezi minane g...

Binti mmoja wa Kipalestina aliyekamatwa baada ya kumchapa kofi mwanajeshi wa Israel amekiri kosa na atatumikia kifungo cha miezi minane gerezani kufuatia maafikiano kati yake na upande wa mashtaka.
Msichana huyo Ahed Tamimi alikiri kuwa na hatia kwa makosa manne aliyokuwa akishtakiwa kati ya 12 yaliyokuwa yakimkabili, ikiwemo shambulio la mwili, wakili wake ameeleza.
Kadhalika, atalipa faini ya shekeli 5,000 sawa na dola 1,440 .
Binti huyo mwenye miaka 17 alikamatwa baada ya kunaswa kwenye picha ya video akiwakabili wanajeshi wawili nje ya nyumba yake mwezi Desemba.
Uamuzi wa mahakama unamaanisha kuwa ataachiwa huru kipindi cha majira ya joto kwa sababu hukumu yake imehesabu siku alizokaa korokoroni, mwanasheria wake Gaby Lasky amenukuliwa na shirika la habari la AFP.
Kwa Wapalestina, Ahed Tamimi, ambaye kwa kipindi hicho alikuwa na miaka 16 wakati tukio lilipotokea Ukingo wa Magharibi, ni ishara ya kutounga mkono makazi ya Israeli.
Lakini waisraeli wanamuona kama mtu mwenye vurugu na kutafuta umaarufu.
Kesi yake ilikuwa ya ndani kwenye mahakama ya kijeshi katika eneo la ukingo wa magharibi tarehe 13 Februari.
Mwanasheria wake alitaka mashtaka hayo yasomwe hadharani lakini Jaji aliamua kesi hiyo iendelee huku ikirekodiwa kwenye kamera.
Ahmed Tamimi alipigwa picha ya video na Mama yake,Nariman, alipokuwa akigombana na wanajeshi wenye silaha, katika kijiji cha Nabi Saleh tarehe 15 mwezi Desemba, baada ya kutokea maandamano yaliyokuwa yakipinga hatua ya Marekani kuutambua mji wa Jerusalemu kuwa mji mkuu wa Israel.
Tukio hilo lililorekodiwa lilikuwa kwenye ukurasa wa Faceook wa Nariman na video ya ugomvi huo ilisambaa sana.Katika video hiyo,Ahed Tamimi alionekana akimpiga teke mwanajeshi mmoja na kumchapa kofi la usoni, na kumtishia kumpiga mwanajeshi mwingine.
Ahed alikamatwa majira ya usiku na kukabiliwa na shutuma 12, kushambulia, kuchochea, kuingilia kazi za wanajeshi na kurusha mawe.
Mama yake pia alishtakiwa kwa makosa ya kufanya uchochezi kwenye mtandao wa kijamii na kushambulia, wakati binamu yake Nour, ambaye alishiriki kwenye tukio hilo alishtakiwa kwa kosa la kushambulia.
Vijana hao pia waliandamana dhidi ya tukio la kumsababishia Mohammed jeraha kichwani.
Kutokana na tukio hilo, Waziri wa Elimu wa Israel Naftali Bennett amesema Ahed na Nour Tamimi wanapaswa kufungwa maisha gerezani.Raia wengi wa Israel wanasema kuwa Ahed Tamimi kwa muda mrefu amekuwa akitumiwa na familia yake, ambayo inashutumiwa kumtumia kuwaghadhabisha wanajeshi Israel.
Ahed kwa mara ya kwanza alikuwa maarufu alipojitokeza hadharani akiwa na miaka 11, alionekana kwenye video nyingine akitishia kumpiga ngumi mwanajeshi mwingine.

COMMENTS

GEOFREY MEDIA TV

https://www.youtube.com/channel/UCChlD-6iNka8I9kmuuZ9MKw
Name

AFRIKA AFYA AJIRA MPYA All Africa News BIASHARA BREAKING NEWS brudani BUNGENI BURUDANI DUNIANI ELIMU FAHAMU HABARI HABARI VIDEO HABARI ZA HIVI PUNDE HUZUNI IKUFIKIE JOB KENYA KIMATAIFA KITAIFA LIFE STYLE MA0NI HURU MAGARI MAGAZETI MAGUFULI MAISHA YA GHARAMA MAJUU MAKALA MAPENZI MASTAA MATOKEO MATUKIO MICHEZO MIKOANI MIX MOHAMMED ALI MOVIE MUBASHARA NAFASI ZA KAZI NEW AUDIO RELATIONSHIP remix REPORT SIASA SIASA KIMATAIFA SOCIAL MEDIA TAARIFA TANZIA TEKNOLOJIA TUNDU LISSU TUZO UCHOKOZI UK NEWSPAPER UKATILI UTAFITI UTANI WA MAGUFULI VIDEO VIDEO MPYA VIDEO:HISTORIA
false
ltr
item
GEOFREY MEDIA: Ahed Tamimi: Binti Mpalestina aliyemzaba kofi mwanajeshi wa Israel afungwa jela
Ahed Tamimi: Binti Mpalestina aliyemzaba kofi mwanajeshi wa Israel afungwa jela
https://3.bp.blogspot.com/-geqTIunohVs/WrQBloKZYoI/AAAAAAAAE44/xYqOu6IotrEDf4A96pJipCoD8LxVplpuwCLcBGAs/s400/_100522249_mediaitem100517080.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-geqTIunohVs/WrQBloKZYoI/AAAAAAAAE44/xYqOu6IotrEDf4A96pJipCoD8LxVplpuwCLcBGAs/s72-c/_100522249_mediaitem100517080.jpg
GEOFREY MEDIA
http://www.geofreymedia.co.tz/2018/03/ahed-tamimi-binti-mpalestina-aliyemzaba.html
http://www.geofreymedia.co.tz/
http://www.geofreymedia.co.tz/
http://www.geofreymedia.co.tz/2018/03/ahed-tamimi-binti-mpalestina-aliyemzaba.html
true
3773606987198414401
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy