Soundcloud

Barcelona yaendeleza ubabe La Liga, Waipoteza Atletico Madrid Camp Nou

Klabu ya Barcelona imefanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya klabu ya Atletico Madrid kwenye mchezo wa mzunguuko wa 27 wa La Liga.
Goli la Barcelona limefungwa na mshambuliaji wake Lionel Messi kwa mpira wa adhabu ya moja kwa moja ambapo hadi dakika 90 zinamalizika goli hilo lilidumu.
Kwa matokeo hayo Barca inakuwa na alama 69 ikifuatiwa na Atletico yenye alama 61 huku Madrid wakishika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa La Liga kwa alama 54.

Post a Comment