Soundcloud

Gumzo lililozuka baada ya ajali aliyoipata Justin Bieber


Siku ya Ijumaa March 23,2018 staa wa muziki kutokea Marekani Justin Bieber alipata ajali jijini Los Angeles ambapo gari lake aina ya Range Rover liligongwa kwa mbele ila upande wa Justin Biebier  hakupata majeraha ya aina yoyote na kutoka salama.
Kutokana na ajali hiyo wengi wameihusisha na mkosi mbaya ambapo alikuwa na msichana kwenye gari hiyo anayefahamika kwa jina la Baskin Champion tetesi zinasema kuwa wawili hao ni wapenzi na hii ni baada ya Justin Bieber kuachana na Selena Gomez.

Taarifa za ajali hiyo ziliwafikia polisi kwa wakati kutokana na magari hayo kuwa na kifaa maalum kwaajili ya kuwafikishia taarifa endapo ajali kama hizo zikitokea.
Justin Bieber na Selena Gomez walionekana kurudisha penzi kati yao mwishoni wa mwaka jana 2017 ambapo Selena Gomez aliachana na staa wa muziki The Weekend.

Post a Comment