http://www.geofreymedia.com/p/wasiliana-nasi.html

Hatuamini uchunguzi uliofanywa na polisi kuhusu Nondo – Mtandao wa Wanafunzi

Mtandao wa wanafunzi nchini Tanzania (TSNP) umesema taarifa walizo nazo za nini hasa kilichomsibu mwanafunzi mwenzao, Abdul Nondo zinakin...


Mtandao wa wanafunzi nchini Tanzania (TSNP) umesema taarifa walizo nazo za nini hasa kilichomsibu mwanafunzi mwenzao, Abdul Nondo zinakinzana na zile zilizotolewa na Jeshi la Polisi baada ya kufanya uchunguzi.
Taarifa za kupotea kwa Bwana Nondo katika mazingira ya kutatanisha ziliibuka tarehe 6 Machi baada ya Nondo kutuma ujumbe kwa mmoja wa marafiki zake usiku wa manane akisema kuwa usalama wake uko hatarini.
Akizungumza na Shirika la Utangazaji la BBC Jumanne hii muda mchache baada ya kutoa ripoti yao juu ya uchunguzi, msemaji wa TSNP Helllen Sisya amesema bado wanasubiri kauli na Nondo mwenyewe ili kujua nini kilitokea.
“Sisi bado hatuamini Uchunguzi uliofanywa na polisi kwa kuwa hatujamsikia Nondo akiongea na kile tulichoelezwa na polisi mkoani Iringa na hiki tulichokisikia leo kwa polisi Dar es Salaam haviendani”, alisema Sisya.
Mtandao wa Wanafunzi Tanzania ambao ulitoa taarifa kwa Umma kuhusu kupotea kwa Abdul Nondo,hawakubaliani na taarifa hiyo ya polisi kwa kudai kuwa inakanganya,Polisi wanadai kuwa alipatikana akiendelea na shughuli zake za kawaida alipoenda kumtembelea mpenzi wake na wakati wao walipata taarifa kutoka kwa jeshi la polisi wa Iringa kuwa Nondo alifika kituoni hapo akiwa hajitambui.
Mapema leo Jeshi la polisi nchini Tanzania lilizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam,Abdul Nondo aliyedaiwa kupotea katika mazingira ya kutekwa ulikuwa uzushi.
Kamanda wa Polisi,Lazaro Mambosasa amedai kuwa taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii na kuzua taharuki mnamo tarehe 6,Machi kwa madai kuwa mwanafunzi huyo ametekwa na watu wasiojulikana si za kweli kwa kuwa uchunguzi wa jeshi la polisi umebaini kwamba mwanafunzi huyo alikutwa akiendelea na shughuli zake za kawaida na wala hakutekwa au kutoa taarifa kuwa ametekwa.
Source:Bongo5

COMMENTS

GEOFREY MEDIA TV

https://www.youtube.com/channel/UCChlD-6iNka8I9kmuuZ9MKw
Name

AFRIKA AFYA AJIRA MPYA All Africa News BIASHARA BREAKING NEWS brudani BUNGENI BURUDANI DUNIANI ELIMU FAHAMU HABARI HABARI VIDEO HABARI ZA HIVI PUNDE HUZUNI IKUFIKIE JOB KENYA KIMATAIFA KITAIFA LIFE STYLE MA0NI HURU MAGARI MAGAZETI MAGUFULI MAISHA YA GHARAMA MAJUU MAKALA MAPENZI MASTAA MATOKEO MATUKIO MICHEZO MIKOANI MIX MOHAMMED ALI MOVIE MUBASHARA NAFASI ZA KAZI NEW AUDIO RELATIONSHIP remix REPORT SIASA SIASA KIMATAIFA SOCIAL MEDIA TAARIFA TANZIA TEKNOLOJIA TUNDU LISSU TUZO UCHOKOZI UK NEWSPAPER UKATILI UTAFITI UTANI WA MAGUFULI VIDEO VIDEO MPYA VIDEO:HISTORIA
false
ltr
item
GEOFREY MEDIA: Hatuamini uchunguzi uliofanywa na polisi kuhusu Nondo – Mtandao wa Wanafunzi
Hatuamini uchunguzi uliofanywa na polisi kuhusu Nondo – Mtandao wa Wanafunzi
https://2.bp.blogspot.com/-LxMqmh7q9iY/WqkCVlUkYTI/AAAAAAAAEs8/50SD38ZCU04TtgBjtVnIfyKG2Wq3J7YpwCLcBGAs/s400/IMG_9948.jpg
https://2.bp.blogspot.com/-LxMqmh7q9iY/WqkCVlUkYTI/AAAAAAAAEs8/50SD38ZCU04TtgBjtVnIfyKG2Wq3J7YpwCLcBGAs/s72-c/IMG_9948.jpg
GEOFREY MEDIA
http://www.geofreymedia.co.tz/2018/03/hatuamini-uchunguzi-uliofanywa-na.html
http://www.geofreymedia.co.tz/
http://www.geofreymedia.co.tz/
http://www.geofreymedia.co.tz/2018/03/hatuamini-uchunguzi-uliofanywa-na.html
true
3773606987198414401
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy