Soundcloud

Marekani na nchi nyingine 3 zafukuza wanadiplomasia wa Urusi


Wiki iliyopita March 17, 2018 serikali ya Uingereza ilitangaza kuwafukuza wanadiplomasia 23 wa nchini Urusi waliokuwa nchini humo baada ya Mpelelezi wa zamani wa Urusi Sergei Skripal na mwanaye Yulia kupewa sumu ya kemikali.
Uingereza inaamini kuwa tukio hilo lilifanywa na Warusi wenyewe, jambo ambalo limefukuza wanadiplomasia hao pamoja na familia zao nchini humo wiki iliyopita.
Sasa leo March 26, 2018 Rais wa Marekani Donald Trump pia amefukuza wanadiplomasia 60 wa Urusi waliokuwa nchini humo Marekani kutokana na scandal hiyo.
Nchi za Ujerumani, Ukrain na Ufaransa pia zimetangaza kuwafukuza wanadiplomasia wa Urusi nchini kwao.

Post a Comment