Soundcloud

Msanii Maua Sama ameeleza sababu ya kuachia picha ambazo si za kawaida kabisa kutoka kwake.

Picha hizo ambazo zilimuacha wazi sehemu kubwa ya mapaja yake aliziweka mtandaoni kati ya February 19 na 22 mwaka huu.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma mpya ‘Nakuelewa’ ameiambia FNL ya EATV kuwa aliachia picha hizo kwa ajili ya ujio wake mpya na pia amefanya hivyo kuonyesha uzoefu wake katika muziki.
“Kiukweli ni photo shoot ambayo nilikuwa nahitaji kwa sababu nilikaa kimya sana,” amesema.
“Kuna ule ugeni sasa umeisha, hivyo nilikuwa mgeni nilikuwa sijui vitu vingi, nilikuwa sijui kwenye muziki natakiwa nifanye nini, kidogo kidogo nikaanza kuzoea mwisho wa siku nikawa vile nilivyokuwa nataka,” amesema.
Licha ya kuwa muimbaji mzuri katika nyimbo zake Maua Sama amekuwa miongoni mwa ma-chorus killer wazuri kwa hapa Bongo, mwishoni wa mwaka jana alisikika katika chorus ya ngoma ya Mwana FA ‘Sielewi’ na ile ya Roma na Stamina (Rostam) itwayo Kiba_100.

Post a Comment