Soundcloud

SIMBA NA YANGA ZATUPWA NJE MICHUANO YA KOMBE LA SHIRIKISHO BARANI AFRIKA - CAF


Wekundu wa Msimbazi Simba safari yao ya kuwania kufuzu kucheza hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la shirikisho barani Africa CAF, imehitimishwa leo katika uwanja wa Port Said nchini Misry baada ya kucheza mchezo wao wa marudiano dhidi ya Al Masry.

Simba SC katika mchezo wa kwanza uwanja wa Taifa Dar es Salaam ikiwa nyumbani ilifanya kosa la kuruhusu kufungwa magoli mawili katika mchezo uliomalizika kwa sare ya kufungana magoli 2-2, hivyo leo walikuwa wanahitajika kupata walau ushindi wa kuanzia goli 1-0 au sare ya kuanzia 3-3.

Kwa bahati mbaya Simba wameshindwa kupata matokeo ugenini dhidi ya Al Masry na kujikuta wakilazimishwa sare tasa (0-0), hivyo kutokana na mchezo wa kwanza wa nyumbani walitoka sare ya 2-2, wanaondolewa katika michuano hiyo kwa goli la ugenini, hivyo sasa amesalia katika michuano ya Ligi Kuu pekee.

Wakati huo huo Yanga SC yaangukia pua katika michuano ya kombe la Shirikisho baada ya kutolewa klabu bingwa Barani Afrika dhidi ya Township Rollers FC huko nchini Botswana.
 

Yanga SC imeyaaga mashindano hayo baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana huku mchezo wa awali uliyopigwa jijini Dar es Salaam ilikubali kipigo cha mabao 2 – 1.
Kwa matokeo hayo sasa timu itatinga kombe la Shirikisho Barani Afrika  kutokana na matokeo yake iliyopata michuano ya klabu bingwa Afrika.
Township Rollers inafanikiwa kusonga mbele hatua ya makundi na kuweka historia hiyo baada ya kuwa na safari ngumu wakati ikiwa imekutana na Al Merkhe kabla ya kukutana na Yanga SC.

Post a Comment