Soundcloud

Azam FC yakwama


Klabu ya soka ya Azam FC imeambulia sare ugenini kwenye mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara uliomalizika jioni hii kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya dhidi ya wenyeji Mbeya City.
Katika mchezo wa leo Azam FC ilipata nafasi kadhaa ambazo imeshindwa kuzitumia vyema hususani katika kipindi cha kwanza ambapo ilitawala mchezo. Kadhalika kwa Mbeya City kipindi cha pili wametengeneza nafasi nyingi lakini wameshindwa kuzitumia pia.
Kwa upande mwingine nahodha wa Azam FC Himid Mao, baada ya mechi ameeleza kuwa wao kama timu wataendelea kupigana hadi mwisho wa ligi na watatumia mchezo wa leo kuweza kufanyia marekebisho matatizo ya ufungaji ambayo yanawanyima ushindi.
Baada ya matokeo ya leo Azam FC imebaki katika nafasi ya 3 ikifikisha alama 45 katika michezo 23. Mbeya City nayo imebaki katika nafasi ya 8 ikiwa na alama 26 kwenye michezo 23. Timu zote zimebakiwa na mechi 7 kabla ya ligi kumalizika.

Post a Comment