Soundcloud

HATIMAYE! MTOTO WA MASOGANGE KUSOMESHWA HADI CHUO KIKUU

MMILIKI wa Shule ya St. Patrick ya Jijini Dar es Salaam, Ndele Mwaselela amejitolea kumsomesha mtoto wa marehemu Agness Gerald ‘Masogange’, Sania hadi elimu ya Chuo Kikuu endapo atafanikiwa kufaulu katika masomo yake.
Sania mwenye umri wa miaka 11 ni mtoto pekee wa Masogange ambaye kwa sasa anasoma darasa la saba, kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa jana Aprili 23, 2018 na Kamati ya Maandalizi ya Mazishi iliyoandaliwa na Bongo Movie.

Jana kamati ya maandalizi ya mazishi kupitia mweka hazina wake, Zamaradi Mketema kueleza kuwa wamemwekea Sh2 milioni zilizobaki katika michango ya msiba huo kwenye akaunti yake. kwa ajili ya kumsaidia kianzio katika cha ada atakapoanza kidato cha kwanza mwakani kwa kuwa mwaka huu anatarajiwa kumaliza darasa la saba.

Post a Comment