http://www.geofreymedia.com/p/wasiliana-nasi.html

Meya aliyesifiwa na Rais afunguka kuhusu kuhama

Meya, Wajiji la Arusha, Kalista Lazaro (CHADEMA) amefunguka na kusema kitendo cha Rais kumsifia mbele ya hadhara ni heshima kwake na vion...


Meya, Wajiji la Arusha, Kalista Lazaro (CHADEMA) amefunguka na kusema kitendo cha Rais kumsifia mbele ya hadhara ni heshima kwake na viongozi wa Arusha na kusema hakuna sababu kiongozi aliyechaguliwa na wananchi kuhama chama kwa kumuunga mkono Rais.
Kalista Lazaro alisema hayo April 7, 2018 baada ya Rais Magufuli kumsifia kuwa ni kati ya watu ambao wanapenda maendeleo na kufanya maendeleo katika jiji la Arusha Mjini licha ya kiongozi huyo kutokea katika chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
"Hii pongezi la Rais ni kwa sababu alipokea taarifa ya utendaji ya jiji la Arusha na tangu alipoingia nilimweleza mambo ambayo tumefanya kwa mfano amepongeza jitihada kubwa ya ujenzi wa madarasa tangu mwaka 2016 ambapo tumejenga madarasa 105, 2017 tumejenga madarasa 61, tunapandisha vituo vya afya mara moja na dispensary kwa ujumla tano, hospitali ya wilaya, barabara za lami, barabara za vumbi na juzi tumetangaza tenda ya kilometa 10 za lami katika jiji la Arusha ambapo barabara ya Njiro, Kwa Mlombo, Sombetini zinaenda kujengwa lami pamoja na barabara ya Ngarenalo kwangu mimi ni heshima na hii heshima nimeipokea kwa niamba ya wananchi wa jiji la Arusha" alisema Kalista Lazaro 
Aidha Kalista Lazaro amedai kupongezwa kwake kuwe funzo kwa viongozi wengine ambao wamekuwa wakihama kutoka CHADEMA na kwenda CCM kwa kigezo cha kuunga mkono serikali na kudai kuwa ukitaka kufanya hivyo unachotakiwa kutekeleza tu yale uliyoahidi kwa wananchi wako na si kwa kigezo cha kuhama chama. 
"Wale ambao walikuwa wanabeza na hawatambui sasa wametambua kuwa Meya wao anapongezwa na Rais Magufuli mbele ya halaiki ya watu, mbele ya polisi, mbele ya Mkuu wa Majeshi hivyo Rais anaona kazi tunayofanya na niwaambie wananchi hakuna sababu ya kiongozi wa kuchaguliwa kuhama, ukitaka kutekeleza wajibu wako na kuunga mkono serikali unatakiwa ufanye kazi ambayo umeahidi wananchi wako. Mimi leo napongezwa nikiwa ndani ya CHADEMA, nikiwa Meya wa CHADEMA na diwani wa CHADEMA kwangu mimi ni heshima" alisisitiza

COMMENTS

GEOFREY MEDIA TV

https://www.youtube.com/channel/UCChlD-6iNka8I9kmuuZ9MKw
Name

AFRIKA AFYA AJIRA MPYA All Africa News BIASHARA BREAKING NEWS brudani BUNGENI BURUDANI DUNIANI ELIMU FAHAMU HABARI HABARI VIDEO HABARI ZA HIVI PUNDE HUZUNI IKUFIKIE JOB KENYA KIMATAIFA KITAIFA LIFE STYLE MA0NI HURU MAGARI MAGAZETI MAGUFULI MAISHA YA GHARAMA MAJUU MAKALA MAPENZI MASTAA MATOKEO MATUKIO MICHEZO MIKOANI MIX MOHAMMED ALI MOVIE MUBASHARA NAFASI ZA KAZI NEW AUDIO RELATIONSHIP remix REPORT SIASA SIASA KIMATAIFA SOCIAL MEDIA TAARIFA TANZIA TEKNOLOJIA TUNDU LISSU TUZO UCHOKOZI UK NEWSPAPER UKATILI UTAFITI UTANI WA MAGUFULI VIDEO VIDEO MPYA VIDEO:HISTORIA
false
ltr
item
GEOFREY MEDIA: Meya aliyesifiwa na Rais afunguka kuhusu kuhama
Meya aliyesifiwa na Rais afunguka kuhusu kuhama
https://3.bp.blogspot.com/-aHpYYFBugvI/Wsok-MMNpRI/AAAAAAAAFK4/rd4WUmzZsMcrDpDOs0JlNorRaHD5RVxZgCLcBGAs/s640/Meya%2BCHADEMA.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-aHpYYFBugvI/Wsok-MMNpRI/AAAAAAAAFK4/rd4WUmzZsMcrDpDOs0JlNorRaHD5RVxZgCLcBGAs/s72-c/Meya%2BCHADEMA.jpg
GEOFREY MEDIA
http://www.geofreymedia.co.tz/2018/04/meya-aliyesifiwa-na-rais-afunguka.html
http://www.geofreymedia.co.tz/
http://www.geofreymedia.co.tz/
http://www.geofreymedia.co.tz/2018/04/meya-aliyesifiwa-na-rais-afunguka.html
true
3773606987198414401
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy