Soundcloud

Mpiganaji mtukutu, Conor McGregor aachiwa kwa dhamana

Mpiganaji wa MMA, Conor McGregor pamoja na wenzake wameripoti kituo cha Polisi cha New York hapo jana siku ya Ijumaa na kuachiwa kwa dhamana baada kuhitajika kufanya hivyo kufuatia kuvamia kikao cha baadhi ya wapiganaji wa UFC  na vyombo vya habari juzi huko Brooklyn na kufanya vitendo vya vurugu hadi kupelekea kuvunja kio cha basi lililokuwa limewapakia wapambanaji hao.

McGregor alitolewa ndani ya jengo la ya idara ya polisi ya New York hapo jana mchana baada ya kuachiwa kwa  dhamana ya dola za Kimarekani 50,000 kwa kutuhuimiwa kufanya makosa matatu ambayo ni ya uhalifu na shambulio la kikatili dhidi ya basi lililokuwa limewapakia watu.

Baada ya mashtaka hayo yanayo mkabili McGregor na wenzie watafikishwa mahakamani mwezi June kuendelea na kesi hiyo wakati wapiganaji wa UFC  wakishindwa kupambana kwenye pambano lao la Jumamosi hii kufuatia wengine kupata majeraha baada ya kushambuliwa na Gregor walipokuwa ndani ya basi hilo.

Post a Comment