Soundcloud

Mtangazaji wa BBC ashambuliwa Twitter kisa nywele


Mtangazaji mmoja wa kipindi cha Breakfast cha Shirika la Utangazaji la BBC, Tina Daheley, 37, amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya watumiaji wa mtandao wa Twitter kumshambulia kwa maneno.
Mtangazaji huyo amesemwa na watumiaji wa Twitter baada ya kupiga picha na kuiweka kwenye mtandao huo, na ndipo watu walipoanza kumsema wakisema kuwa mtindo wa alivyobana nywele zake hauko kitaalamu.
Hivyo wamemshauri mtangazaji huyo Daheley kuzibana nywele zake vizuri akiwa anatangaza na sio kuzichia, kwani haziendani na misingi ya taaluma yake.
Source:Millardayo

Post a Comment