Soundcloud

Ronaldo apoteza matumaini ya Juventus kusonga mbele UEFA


Klabu ya Real Madrid jana usiku imeibuka na ushindi mnono wa goli 3-0 dhidi ya Juventus, mchezo uliopigwa nchini Italia na kupoteza kabisa matumaini ya Vizee wa Torino kusonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa barani ulaya.
Magoli ya Real Madrid yalifungwa na Cristiano Ronaldo x2 na moja likifungwa na Marcelo kunako dakika 72 .
Kwa matokeo hayo Juventus ina kibarua kigumu cha kupata matokeo ya goli 4-0 au ushindi wowote wa tofauti ya goli 4 ili waweze kusonga mbele  kwenye michuano hiyo kitu ambacho kitakuwa kigumu sana kwao.
Hata hivyo, Juventus itakuwa na wakati mgumu zaidi kwani kwenye mchezo wa marudiano  itamkosa mshambuliaji wake Dyabala baada ya jana kwenye mchezo huo kupata kadi nyekundu.
Matokeo mengine ya jana ni ushindi wa Bayern Munich wa goli 2-1 dhidi ya Sevilla mchezo ambao ulikuwa na msisimko sana kutokana na ugumu wa timu zote mbili kwenye safu ya ulinzi.

Post a Comment