Soundcloud

Steve Nyerere ahoji Ray, JB, Aunt Ezekiel, Shamsa Ford, Johari, Uwoya, Batuli kutopatiwa Tuzo


Baada ya utoaji wa Tuzo za filamu za Sinema Zetu International Film Festival Awards (SZIFF), msanii wa filamu Bongo, Steven Nyerere amesema atazungumza baada ya kuona baadhi ya wasanii ambao anaona walistahili kupata lakini haikuwa hivyo.
Muigizaji huyo amehoji kwanini waigizaji wakubwa kama Ray Kigosi, JB, Aunt Ezekiel, Shamsa Ford, Johari na wengineo kutokuwepo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;
“Nitaongea nilichokiona kwenye tuzo, kwanini Ray, JB, Rich, Roams, Aunt Ezekiel, Shamsa Ford, Duma, Weru, Hemedi, Tausi Mndengela, Mainda, Johari, Uwoya, Marian Ismail, Batuli na wengine wanaofanya vizuri wapo wapi ?,” amehoji.
“Na mbona sijawaona na kuna vijana wasanii chipukizi wanafanya vizuri, nini tatizo,” ameongeza.
Katika Tuzo za filamu za Sinema Zetu International Film Festival Award (SZIFF) zilizotolewa April Mosi mwaka huu, miongoni mwa waigizaji waliofanya vizuri ni pamoja na Gabo Zigamba aliyejinyakulia tuzo tano wakati Wema Sepetu alishinda tuzo mbili.

SOURCE:BONGO5

Post a Comment