Soundcloud

The Weeknd atoa onyo kwa Wizkid na wasanii wengine wanaotumia neno ‘StarBoy


Msanii wa muziki kutoka Canada, The Weeknd amewaonya wasanii wa muziki dunia akiwemo Wizkid kuacha mara moja kutumia neno ‘StarBoy’ kwa madai kuwa neno hilo ameshalilipia (TradeMark) kwa matumizi yake ya kibiashara.
The Weekend amesema kuwa yeye ndiye muanzilishi wa neno hilo ‘StarBoy’ na yeyote atakayetumia atachukuliwa hatua za kisheria.
Kwa mujibu wa mtandao wa Burudani na Mastar TMZ, Tayari wanasheria wa The Weeknd wameshaandaa nyaraka za kumburuza Eymun Talasazan mahakamani kwa kutumia neno ‘StarBoy’ kwenye vipindi vyake vya TV baada ya The Weeknd kuachia album yake ya ‘StarBoy’ mwaka 2016.
Wimbo wa ‘StarBoy’ ni moja ya nyimbo zilizopo kwenye album hiyo na ulifanikiwa kushika namba moja kwenye chati za Billboard top 100.
Kwa The Weeknd wimbo wa StarBoy ni wimbo wa tatu kushika namba moja kwenye chati hizo maarufu zaidi duniani.
Bonyeza PLAY kuitazama Video ya The Weekend ya Wimbo wake wa Starboy 

Post a Comment