Soundcloud

Alichozungumza wakala wa Yaya Toure kuhusu Guardiola na Toure kuondoka

Baada ya kiungo wa Man City Yaya Toure kuagwa rasmi na wachezaji na viongozi wa timu ya Man City baada ya kudumu katika club hiyo kwa miaka nane toka alipojiunga nayo mwaka 2010 akitokea club ya FC Barcelona ya Hispania, wakala wake Dimitri Seluk ameongea na kuweka wazi anachokiamini.


“Yaya alikuwa ni moja kati ya wachezaji wa mwanzoni kusainiwa na Man City wakati Sheikh Mansour alipoamua kuifanya Man City kuwa club kubwa na Yaya amefanya vizuri Man City lakini leo sio ndio mwisho wa kucheza soka kwa Yaya Toure bado ataendelea kucheza England na atadhihirisha kuwa anaweza kucheza kwa kiwango kikubwa”Dimitri

Post a Comment