Soundcloud

Kampeni kubwa yaanzishwa kumzima R.kelly

Msanii Robert Sylvester Kelly ambaye ni muimbaji, mwandishi wa nyimbo,mzalishaji wa muziki, na mchezaji wa zamani wa mchezo wa kikapu yuko matatani kutokana na kampeni kubwa ambayo imeanzishwa dunia nzima kwa lengo la kumzima msanii huyo kutokana na vitendo vyake vya uzalilishaji wa wanawake. 

Kampeni hiyo ya #muteR.kelly iliyoanzishwa na The women of color in the Time’s Up organization imeomba media zote duniani zikiwemo Blog, tv station, radio station, kutokupiga nyimbo zake wala kumpa nafasi yoyote kimuziki huku wakiomba watu wote duniani kutonunua kazi zake katika platform zinazouza  muziki wa R.kelly duniani hatua itakayomuondoa kabisa msanii huyo katika Ramani ya muziki duniani.

Wanaharakati mbalimbali nchini marekani na duniani akiwemo Tarana Burke,Ava DuVernay na Shonda Rhimes wameunga mkono kampeni hiyo huku wakiomba uchunguzi ufanyike kuhusiana na tabia ya msanii huyo kuwazalilisha wanawake wenye umri mdogo.Mwaka 1994 R.kelly akiwa na miaka 28 alimuoa msanii wakike marehemu Aliyah Dana Haughton ambaye alikuwa na miaka 15 na hapo ndipo mfalme huyo wa R&B duniani alianza kukosolewa na kupingwa vikali.
Hata hivyo uongozi wa R.Kelly umesema unaanda utaratibu wa kupinga Kampeni hiyo kwa madai ni ya uongo na inalengo la kumchafua msanii huyo.
Ikumbukwe ni kwa miongo miwili sasa mfalme huyo wa R&B duniani amekuwa akiandamwa na kashfa za uzalilishaji wa kingono kwa wanawake wenye umri mdogo huku wanawake hao akiwafanyia vitendo mbalimbali kinyume na matakwa yao.

Wachambuzi wa mambo wamesema salama ya msanii huyo nikujirudi na kukaambele ya media mbalimbali kuomba radhi na kulipa fidia kwa wanawake wote aliowafanyia udhalilishaji huo.
               Waweza tazama Makala hii fupi kuhusu kampeni hiyo hapo chini.......

Post a Comment