Soundcloud

Singida United yamtangaza Mbrazili wake, Do Santos na wachezaji wengine wawili


Uongozi wa klabu ya Singida United imewatambulisha rasmi wachezaji wake watatu waliyo wasajili kwaajili ya michuano ya mbali mbali inayoikabili timu hiyo changa iliyopanda daraja msimu uliyopita.


Wachezaji waliyo tambulishwa hii leo siku ya Alhamisi ni mshambuliaji raia wa Brazili, Felipe Olveira do Santos , Amara Diaby raia wa Ivory Coast pamoja na Tiba John George anaetokea klabu ya Ndanda FC.

Wachezaji hao wametangazwa jijini Arusha wakati, Tiba John kutoka Ndanda FC akisaini kandarasi ya miaka mitatu, Mbrazili, Do Santos na Muivory Coast, Amara Diaby wakitokea klabu ya Asec Mimosa ya nchini Ivory Coast.

Post a Comment